GET /api/v0.1/hansard/entries/968920/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 968920,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/968920/?format=api",
"text_counter": 466,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kaloleni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Paul Katana",
"speaker": {
"id": 13357,
"legal_name": "Paul Kahindi Katana",
"slug": "paul-kahindi-katana-2"
},
"content": " Asante Mhe. Spika wa Muda. Nasimama kuunga mkono Ripoti hii. Ukiangalia Ripoti hii na vile hali ilivyo kwa sasa, Wizara ya Uchukuzi imezembea na inachezea maisha ya wananchi ambao wanatumia kivuko cha feri cha Likoni. Tunaweza kulaumu Mkurugenzi na timu yake ambao wako kwa feri, lakini hawana fedha za kufanyia ukarabati feri hizi. Ukiangalia feri ya MV Harambee ambayo ilihusika kwa ajali, MV Nyayo na MV Kilindini, zina umri wa miaka 30. Tunatumia pesa nyingi. Feri moja inatumia zaidi ya Kshs100 milioni kufanyiwa ukarabati."
}