GET /api/v0.1/hansard/entries/969319/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 969319,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/969319/?format=api",
    "text_counter": 395,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Likoni, ODM",
    "speaker_title": "Mhe. (Bi.) Mishi Mboko",
    "speaker": {
        "id": 874,
        "legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
        "slug": "mishi-juma-khamisi"
    },
    "content": " Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda. Kwanza nataka nishukuru sana Bunge hili kwa sababu kupitia kamati ya PIC, waliweza kuona kwamba suala la usalama wa Wakenya katika Kivuko cha Likoni ama kupitia zile feri ni muhimu. Kamati hiyo ilitembelea kivuko kile na kutathmini changamoto zilizoko pale. Kwa hivyo, ni shukrani sana kwa Mwenyekiti wa PIC pamoja na wanachama wake na Bunge kwa ujumla. Kivuko cha Likoni kinaunganisha taifa la Kenya na Jamhuri ya Tanzania, nchi jirani ambayo tuko nayo katika Muungano wetu. Kuhusu changamoto ambazo ziko pale, kuna takriban feri sita ambazo zina matatizo makubwa sana. Hususan, ni feri moja iitwayo MV Harambee. Feri hiyo ndiyo ilihusika katika ajali ambayo tulimpoteza dada yetu pamoja na mwananwe. Ni feri ambayo haitakikani kuwa inahudumu kwa sababu ina matatizo zaidi ya kumi na mawili. Inapaswa kufanyiwa ukarabati wa kutosha. Kama taifa, kupitia taasisi ya KPA, tuna uwezo wa kuwa na kituo chetu cha kufanya ile tunaita kwa Kiingereza “dry dock services”, yaani kupata zile huduma za kufanya ukarabati wa vifaa vyetu vya baharini—iwe ni feri, iwe ni meli, ama hata zile boti zetu ambazo tunatumia - badala ya kutumia pesa nyingi sana katika kampuni ya African Marine ambayo inatufanyia kazi ambayo pia haiwezi kuwa sawa na kiwango kile kinachotakikana. Jambo la tatu katika ripoti hii, waligundua kwamba hata wale wahandisi wa baharini wanaofanya kazi pale, ama wale tunaita cockswain, hawana tajriba kamili ya uhandisi wa baharini. Hivyo basi pia, hiyo ni changamoto. Tuweze kupata watu ambao wana tajriba ya juu ya uhandisi wa baharini ili waweze kufanya huduma kwa njia inayofaa. Sharti kuwepo na ukaguzi wa feri wakati unaofaa ili tuweze kutathmini changamoto zilizoko katika zile feri zetu. Katika kutatua matatizo ya dharura ama ajali ambazo zinatokea mara kwa mara, ajali za kupoteza maisha ya watu ama ajali za kupoteza mali kupitia zile lori na kanta ambazo zinabeba mali tofauti hata zile zinazotoka katika nchi jirani ya Tanzania, tunahitaji tuwe na zile tunaita"
}