GET /api/v0.1/hansard/entries/969323/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 969323,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/969323/?format=api",
"text_counter": 399,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Mhe. (Bi.) Mishi Mboko",
"speaker": {
"id": 874,
"legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
"slug": "mishi-juma-khamisi"
},
"content": "kuisaidia kwa kuinyanyua. Iwapo tungekuwa nazo, ile ajali iliyotokea kule kivuko cha Mtongwe miaka iliyopita na kupelekea sisi kupoteza watu takriban 250 isingekuwa mbaya kiasi hicho. Vile vile, tunahitaji kuwa na wapiga mbizi ambao wana tajriba ya kusaidia haswa wakati kumekuwa na dharura kama ile. Tuweze kupata vijana ambao wana ujuzi wa kuogelea baharini.Wawe ni watu wanaoelewa bahari na wanaweza kuwa wakombozi wakati kunapotokea ajali. Tunataka pia tuweze kuwa na vile vifaa ambavyo vinahitajika haswa katika vivuko vya feri. Kwa mfano, maboya ambayo yanaweza kusaidia katika hali ya usalama wakati kunatokea hali ya dharura. Lazima pia tuwe na vifaa vya welding ambavyo vitakuwa pale kwa shida yoyote. Tumeona kwamba feri zile zote zina milango ambayo imeisha nguvu. Milango hiyo inaweza kuzama wakati feri inaegeshwa. Milango hiyo ama bamba la feri (zinavyojulikana kule mitaani) inahitaji ukarabati wa hali ya juu. Hivyo basi, lazima ile feri mpya ambayo Wakenya wamenunua kupitia pesa tulizotenga katika Bunge letu, iletwe haraka. Itatumika wakati nyingine zinafanyiwa ukarabati. Tunapaswa kuwa na mtandao wa mawasiliano ambao utaunganisha zile taasisi muhimu zote ili kusaidia wakati wa dharura. Taasisi hizo ni kama KPA, KMA, Coast Guards na Kenya Navy. Kwa sababu taasisi hizi zote ziko katika eneo moja na ni taasisi ambazo zinahusika na mambo ya bahari na mambo ya vyombo vya baharini. Kwa hivyo, iwapo taasisi hizi zitakuwa na mawasiliano wakati wa dharura, mbiu itakapopigwa iwapo kumekuwa na dharura, basi tunaweza kupata msaada wa kusaidia Wakenya wengi ambao wako pale. Vile vile, tunahitaji ushirikiano wa washikadau wa taasisi hizo. Iwapo taasisi hizi zitakuwa na ushirikiano dhabiti, ushirikiano wa kuangalia utendaji kazi wa vivuko hivi ama vile vivuko kule sehemu za Nyanza ambapo pia kuna feri, basi tutaona huduma hizi na pia mapato katika taifa letu la Kenya yataweza kuongezeka. Wizara ya Uchukuzi sharti itilie maanani ile ajenda ya kuwa na miundo misingi ya kuweza kusaidia kivuko cha Likoni, kivuko cha Mtongwe na vivuko vinginevyo. Tunahitaji muundo msingi kama ule wa Dogo Kundu Bypass. Nataka kushukuru Serikali ya Kenya kwa sababu imeanza barabara ile na hivi karibuni, itamalizika. Vile vile, kuna azma ya kutengeza daraja katika Kivuko cha Likoni. Daraja hili litakapowekwa, litatupunguza maafa mengi. Pia litasaidia uchumi wa kaunti za Kwale na Mombasa haswa mji wa Likoni. Tunajua uchumi wetu unategemea utalii. Iwapo kivuko kile kitakuwa na changamoto ambazo zitapotezea watu wakati, basi uchumi hautaweza kuwa sawa. Serikali lazima izingatie kupanga bajeti vilivyo. Sisi Wabunge, lazima tuangalie bajeti zetu tunazipanga vipi. Kila wakati taasisi hizi zinapoomba pesa, tunazipa pesa kidogo sana. Wakati wameomba Ksh199 milioni, unaona wamepatiwa Kshs76 milioni. Kwa hivyo, wamekuwa wakipata pesa chache ambazo haziwezi kuwasaidia kutoa huduma bora. Kwa hivyo, tunasema wakati tunatengeza bajeti zetu, lazima tuzingatie hilo. Bodi hivi sasa imevunjwa. Lakini iwapo tunaunda bodi nyingine, lazima tupate hata kama sio wanachama wote, tupate baadhi ya wanachama ambao wana tajriba ya uhandisi wa baharini ama wana tajriba ya mambo ya vivuko vya bahari, mambo ya usafiri wa bahari na mambo ya vyombo vinavyotumika baharini. Kwa sababu anayevaa kiatu ndiye anayejua kiatu kinamfinya wapi. Iwapo bodi nzima itakuwa ni watu ambao hawajui, hawaelewi, hawana ufahamu, basi tutaendelea kuwa na matatizo. Hata yule ambaye atasimamia taasisi ile lazima awe mtu ambaye ana tajriba ama anaweza kuelewa haswa mambo ya uhandisi wa baharini."
}