GET /api/v0.1/hansard/entries/969325/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 969325,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/969325/?format=api",
    "text_counter": 401,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Likoni, ODM",
    "speaker_title": "Mhe. (Bi.) Mishi Mboko",
    "speaker": {
        "id": 874,
        "legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
        "slug": "mishi-juma-khamisi"
    },
    "content": "Ikiwa hatutakuwa na mambo kama hayo, basi tutakuwa na changamoto nyingi sana. Pia, taifa letu la Kenya limeungana na nchi nyingi sana katika mambo ya baharini. Inabidi tuweke taasisi ambazo pia, hata wale wafanyikazi wetu wanaweza kupata elimu na taaluma za kuwawezesha kuboresha hali zao za kazi. Pia, elimu kwa mwananchi na usalama wake wakati anatumia vivuko kame vile iwe inarudiwa kila wakati katika kivuko kile kupitia vile vyombo vya mawasiliano kukumbusha Wakenya kwamba wanapoingia ndani ya feri, wazime magari zao na iwapo wako ndani ya gari, watoke nje na wasimame bambizoni mwa feri. Mambo kama yale yanafaa kuingiliwa. Vile vile, kuna kile chombo kinachoitwa chain kwa Kimombo ambacho kina wekwa nyuma wakati magari yameingia katika feri. Lazima vifaa kama vile viweze kupatikana. Hii ni kwa sababu juzi tu dada yetu Kighenda, gari lake lilizama kwenye bahari."
}