GET /api/v0.1/hansard/entries/969339/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 969339,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/969339/?format=api",
    "text_counter": 415,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lungalunga, JP",
    "speaker_title": "Hon. Khatib Mwashetani",
    "speaker": {
        "id": 2163,
        "legal_name": "Khatib Abdallah Mwashetani",
        "slug": "khatib-abdallah-mwashetani"
    },
    "content": "Kwanza, ninatoa pongezi kwa Kamati ambayo inaongozwa na Mhe. Sharriff Nassir kwa kuweza kuja na Ripoti hii ambayo kusema ukweli, siyo Ripoti ambayo itatumika kwa sababu ya majanga yaliyotokea kwa vivukio vya feri. Lakini Ripoti hii inaweza kutumika kwa njia zote kuhakikisha kuwa usalama wetu umedumishwa na vitengo ambavyo vimepewa nafasi hii. Feri hizi zetu kila siku pale kuna watu zaidi ya 300,000 wanaovukishwa na vivukio hivyo. Vile vile, kuna magari zaidi ya 6,000. Hiyo ni idadi kubwa sana ambayo ni muhimu iangaliwe kwa urefu. Ni mengi ambayo yamedokezwa katika Ripoti hii ambayo sisi kama Wajumbe na wale ambao ni wahusika tulikuwa hatufahamu wala hatuelewi. Wakati kulitokea janga lile, wengi tulinyooshea kidole wale wasimamizi wa halmashauri ile. Lakini ukiangalia Ripoti hii, kulingana na mipango ya Kenya Ferry Sevices ni kuwa kila feri inatakikana itumike kwa miaka 20. Lakini ukiangalia katika Ripoti hii, MV Harambee ilitengenezwa 1990. Iko na miaka 30 mpaka leo. MV Likoni ilitengenezwa mwaka wa 2010, na vile vile iko na miaka kumi."
}