GET /api/v0.1/hansard/entries/969393/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 969393,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/969393/?format=api",
"text_counter": 469,
"type": "speech",
"speaker_name": "Tana River CWR, MCCP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Rehema Hassan",
"speaker": {
"id": 13275,
"legal_name": "Rehema Hassan",
"slug": "rehema-hassan"
},
"content": " Ahsante Naibu Spika wa Muda. Nataka kumpa kongole Mheshimwa K’oyoo kwa kuleta Hoja hii ya muhimu kwa Wakenya wote. Mafuriko hapa Kenya yamekuwa ni janga kuu haswa kwa wale tunaotoka sehemu tambarare. Nasema kwa Serikali kuwa shida zingine zinaweza tatuliwa. Kwa mfano, sehemu ninaotoka ni tambarare kweli lakini kule Tana River tuna barabara za maji. Barabara hizo zinaezajengwa ili maji yasipite huko kwa wengi. Kwa mfano, katika eneo la Madogo sehemu ya Ziwani iko ng’ambo ya mto sehemu ya Garissa, barabara ya maji ni ndogo sana sehemu hiyo. Serikali ikichukua hatua inaweza kuzuia maji yasiingie kwa miji."
}