GET /api/v0.1/hansard/entries/969394/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 969394,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/969394/?format=api",
"text_counter": 470,
"type": "speech",
"speaker_name": "Tana River CWR, MCCP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Rehema Hassan",
"speaker": {
"id": 13275,
"legal_name": "Rehema Hassan",
"slug": "rehema-hassan"
},
"content": "Kiswahili chasema kuwa ni heri kuziba ufa kuliko kujenga ukuta. Yatakikana tuwe tunayapangilia mambo kama hayo kama mitigation. Ni muhimu sana. Tunajua mapema kuwa hadhari hizi ziko miaka nenda miaka rudi. Lazima tujipange. Saa hii sehemu kubwa ya Tana River iko ndani ya maji. Mimea iko ndani ya maji na nyumba zimebomoka. Pia naomba wasamaria wema waende kwa sehemu zimehadhirika kama Tana River, Pokot na zingine wapeane misaada kwa watu wanaoumia. Kuna watu wanalala kwenye nyumba ambazo wamezifunika na nguo zao. Hawana hema. Ni vizuri wafikishiwe hema, chakula na hata madawa."
}