GET /api/v0.1/hansard/entries/969415/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 969415,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/969415/?format=api",
    "text_counter": 491,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
    "speaker": {
        "id": 786,
        "legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
        "slug": "ruweida-mohamed-obo"
    },
    "content": "Mwaka jana, mafuriko yalitokea nakulikuwa na mipango ya waathirika kulipwa. Kamati ilipendekeza lakini mpaka leo, hawajalipwa. Yale yaliyotokea sasa yametokea zaidi mengine. Kila mwaka sasa yamekuwa yakitokea. Hawa wafugaji wanapata matatizo sana kwa sababu hali ya hewa imebadilika. Ikiwa si mafuriko ni ukame. Ukame unatokea na ninashukuru Serikali. Ilikuwa na jitihada kutumia shirika la Kenya Meat Commission (KMC). Ninashangaa kama hili Shirika linajua ramani ya Kenya kwa sababu walienda kaunti zingine zote wakaokoa wafugaji, wakachukua ile mifugo, wakachinja wakasaidia wale ambao hawana chakula, lakini Lamu hawakufika. Sijui ramani ya Lamu inakaa vipi, ni watu hawaielewi ama wanaona hawa ni wanyonge wazidi kukandamizwa maanake wafugaji wa Lamu hawakupata kusaidika na hili shirika la KMC. Wengine wengi wamesaidika lakini hao hawakusaidika. Saa hii watu wengine wanalipwa kwa ile mifugo waliotoa wakati wa ukame ilhali watu wangu wa Lamu wametatizika. Ukweli ni kwamba Lamu ni kaunti ambayo ina wafugaji. Sehemu ya Witu kuna upande mkubwa, jamii ya Orma wako hapo na wana mifugo wengi."
}