GET /api/v0.1/hansard/entries/969806/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 969806,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/969806/?format=api",
"text_counter": 348,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "kwenye County Assembly ya Kiambu kwa sababu kungekuwa na mtafaruku. Hapa leo amepewa fursa ya kujitetea, lakini akatoa taarifa bila kula kiapo. Swala lililokuwa hapa ni kwamba kulikuwa na ushahidi kwa kiapo kusema kwamba yeye amemuoa bibi anayeitwa Susan Wangui Ndung’u, mke wake wa ndoa kwa kulingana na mila za Kikuyu. Wakataja watoto wake kwamba wamehusika katika kupewa zabuni katika Kaunti ya Kiambu wakati yeye kama gavana alikuwa hukustahili kutoa zabunii kwa watu wale. Ushahidi huu wote upo katika mikono ama korti ya mwananchi. Hii ina maana kuwa ni ushahidi ambao ni wa uhakika wakuweza kumpata na hatia. Bw. Spika, sisi hatuungi mkono upande wowote. Mashtaka yalikuwa ni dhidi ya Gavana Waititu na Bunge la Kaunti ya Kiambu. Kwa hivyo suala liloko hapa ni kwamba maamuzi yetu lazima yazingatie sheria na maswala ambayo yako mikononi mwa wananchi. Katika mahakama ya mwananchi, mtu anapokataa kula kiapo ni kwamba hasemi ukweli kwa sababu yeyote ambaye anakula kiapo anatakikana kusema ukweli. Kwa hivyo, alipoulizwa kula kwamba yaliyofanyika siyo sawa, Gavana Waititu aliamua kutoa taarifa tu bila ya kuapa. Kwa hivyo, yale yote ambayo yalizungumzwa kwa kiapo, ni mambo ambayo hayakupingwa na kulingana na sheria ni kwamba yale mashtaka yote matatu ambayo yamezungumziwa yamepita."
}