GET /api/v0.1/hansard/entries/969823/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 969823,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/969823/?format=api",
"text_counter": 365,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Bw. Spika, jambo la kwanza ni kuwa mawakili wa Gavana Waititu waliofika hapa hawakuweza kuweka wazi stakabadhi zao za utetezi wake kulingana na mashtaka ya Serikali ya Mashinani ya Kiambu. Bw. Spika, walipoulizwa ni kwa sababu gani hawakufanya hivyo, wakasema wao walikuwa tayari kumtetea Gavana mbele ya Seneti. Walimwambia Gavana kuwa watakuja hapa na kutwaambia kupitia Preliminary Objection (PO) kuwa Seneti haina haki ya kusikiliza mashtaka au kesi ambayo imewakilishwa na Bunge la Kaunti ya Kiambu. Hapo ninaona ya kwamba walijaribu kujinyoa wenyewe na badala ya kumtumikia Gavana wao walikuwa wanatumikia nafsi zao. Kawaida ya sheria ni kuwa mtu akileta stakabadhi za kujitetea, anaruhusiwa pia kuleta PO yake ya kujitetea. Baadaye anahitajika kuuliza PO yake isikilizwe kabla ya kesi yenyewe kusikilizwa. Hii ni kwa sababu itasaidia uhahamisisho wa kesi yake. Lakini jambo hilo halikuwezekana na Gavana Waititu. Kwa hivyo, wao walijikata miguu na hawana mtu yeyote wa kulaumu. Bw. Spika, ninatoka katika eneo la Pwani ambalo lina matitizo mengi ya mashamba. Ni aibu kuona mtu kama Gavana ananyang’anya mama mjane shamba lake halafu baada ya kujulikana alifanya hivyo analilirejesha. Sasa sheria inasema ya kwamba si swala la kulirejesha shamba ambalo ni muhimu sana na kwamba hukufanya makosa. Sheria inaadhibu ile nia ya uhalifu. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}