GET /api/v0.1/hansard/entries/969859/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 969859,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/969859/?format=api",
    "text_counter": 401,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii. Sauti ninazosikia hapa zinasema “tumsulubishe Gavana Waititu”. Lakini, swali ninalojiuliza ni Hoja hii ilipofika hapa kama ilitumia njia inayofaa na viwango vinavyohitajika katika kaunti zetu? Kama Mwenyekiti wa Kamati ya Ugatuzi, sheria zetu zinasema kinagaubaga na dhahiri ya kwamba kunapaswa kuwa na kiwango fulani ya Wabunge wa Kaunti. Lakini kama kulingana na wakili alivyouliza maswali, ikiwa kile kiwango hakikufikishwa, je, sisi kama Seneti tunapaswa kusikiza Hoja hii? Itakuwa jambo la kuvunja moyo wakati swala hili litapelekwa kortini. Sisi tutaulizwa kwa nini hatukufanya vile inapaswa kuwa. Ninauoga na ninatetemeka. Ni vizuri tufuate mfano mwema. Tulipokuwa tunaongea hapa na kura ilipopigwa, tulisema ya kwamba hatutapatiana muda zaidi kwa sababu muda umekwisha lakini sisi wenyewe hatufuati sheria. Kama vile mzungu anavyosema, what is good for the goose must begood for the gander . Tunapaswa kutumia Hoja hii-"
}