GET /api/v0.1/hansard/entries/969870/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 969870,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/969870/?format=api",
"text_counter": 412,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Boy",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13200,
"legal_name": "Issa Juma Boy",
"slug": "issa-juma-boy"
},
"content": "Asante, Mheshimiwa Spika, kwa kunipa fursa hii. Sitachukua muda mwingi; nitachukua dakika mbili au moja na nusu. Tumesikia mahojiano kutoka upande wa Gavana Waititu na Kaunti ya Kiambu. Ninaomba kuwaambia Maseneta wenzangu kwamba kuna mambo mengine, kwa mfano, tunaposafiri katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, Nairobi au Mombasa kama viongozi, tukifika pale tunavua saa, mkanda na viatu kwa sababu tunaheshimu sheria na ofisi zetu. Kwa hivyo, kama umepewa madaraka kama gavana au Mbunge, unafaa kufuata sheria. Bw. Spika, ardhi ya mama mjane ilichukuliwa na mtu ambaye alikuwa kwenye madaraka ambayo ni makosa. Wewe kama mwananchi umepewa wadhifa ili ufanye kazi yako. Kwa hivyo, naunga mkono Hoja ya kumnga’tua Gavana Waititu kutoka kwa ofisi. Sio kwa sababu za kisiasa. Hoja yenyewe imeeleza wazi. Ukiangalia upande wa matumizi wa kifedha na wakuajiri watu, kuna matatizo. Kwa hivyo, katika shughuli ya leo, Kenya nzima inatuangalia. Kwa hivyo, tuwe na msimamo moja ili tuamue kama Maseneta iwe funzo kwa watu wote na ionekane kwamba Seneti ya Kenya inafanya kazi na inatambua shida za wananchi."
}