GET /api/v0.1/hansard/entries/970/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 970,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/970/?format=api",
    "text_counter": 475,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 96,
        "legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
        "slug": "johnson-muthama"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, nashukuru kwa nafasi hii ili niweze kuchangia jambo hili, ambalo ni la muhimu sana na limeweza kuishtua nchi nzima. Mimi mwenyewe niliweza kufika kwenye vikao vilivyokuwa vikiendeshwa na Mwenyekiti hapa, na nilipata nafasi na fursa ya kuweza kusikiza maoni ya wananchi. Vile vile, mimi mwenyewe niliweza kutoa uamuzi wangu. Bw. Naibu Spika wa Muda, jambo hili lilikuwa ni jambo zito mno na liliumiza nchi nzima; wakenya walipatwa na machungu na hasira kubwa sana. Cha kutia aibu na shaka kubwa ni kwa sababu tangu hawa wananchi wafike katika sehemu walizojenga nyumba zao, ukweli wa mambo ni kwamba hawakujenga zile yumba kwa siku moja, siku mbili, hawakujenga kwa mwezi mmoja, bali walijenga kwa miezi kumi na mine au zaidi."
}