GET /api/v0.1/hansard/entries/971/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 971,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/971/?format=api",
    "text_counter": 476,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 96,
        "legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
        "slug": "johnson-muthama"
    },
    "content": "Ni jambo la aibu kuona ya kwamba mambo haya yalifanyika machoni mwa naibu wa chifu, DO, DC na Mkuu wa Mkoa. Hawa wote ni waakilishi wa Serikali mashinani. Maofisa hawa wangeweza kujulisha Serikali juu ya uvamizi wa shamba hili. Kama wangefanya hivyo, basi wananchi wengi hawangejipata matatani ya kununua shamba bandia. Mimi ninapinga vikali uvamizi wowote wa mashamba ya umma na watu binafsi. Hata hivyo, jambo ambalo sikubaliana nalo ni ubomoaji wa nyumba za watu. Nyumba hizi ziliwagharimu watu hawa mamilioni ya pesa. Hii ilikuwa ni mijengo ya kifahari na ilijengwa kwa muda wa miaka mingi. Ni fedheha ilio je kuona nyumba hizi zikibolewa bila ya notisi kutolewa!"
}