GET /api/v0.1/hansard/entries/971153/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 971153,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/971153/?format=api",
"text_counter": 243,
"type": "speech",
"speaker_name": "Igembe South, Independent",
"speaker_title": "Hon. John Paul Mwirigi",
"speaker": {
"id": 1574,
"legal_name": "Cyprian Kubai Iringo",
"slug": "cyprian-kubai-iringo"
},
"content": "kuwashughulikia wazee. Wakati mwingine, wazee hutafuta haki kwenye mahakama yetu lakini hawapati. Ni kana kwamba hawana haki kwa ajili ya umri wao mkubwa. Huu Mswada utawasaidia sana wazee kwa maana unajali maslahi yao. Kuna pendekezo limetolewa kwenye Mswada huu linaloashiria kuwa Kaunti ziweze kutengeneza orodha ya wazee na kuwasajili. Hivyo basi, kila familia iliyo na mzee itajulikana. Kwa jinsi hiyo, Serikali itajua wazee walio kwenye familia hizo. Afya ni kitu cha muhimu lakini wazee hawawezi kupata bima ya afya. Kwa kuwaorodhesha, Serikali itajua ni familia zipi zilizo na wazee na hata kujua hali yao ya kiafya. Itaweza kuwashughulikia kwa njia nzuri. Wazee wengi wanaaga dunia kwa sababu hakuna watu wanaojali hali yao. Katika familia nyingi, vijana wamewageuka wazee kiasi cha kuwachapa kwa ajili ya mashamba. Kuna ugomvi mwingi kuhusu mashamba na vijana wanawafurusha wazee kutoka kwenye mashamba yao. Mswada huu utawapa wazee nafuu kwa sababu shida zao zitashughulikiwa. Hata wakipeleka lalama zao mahakamani, watasikilizwa. Kesi kuhusu mashamba yao zitaamuliwa. Wazee hawana nguvu ya kupigana na vijana wao. Hii sheria ikipitishwa, itawashughulikia na hakuna mtu ataingilia maslahi yao. Kuna wale wazee ambao wako na miaka sitini kuenda juu ilhali hawana vitambulisho. Wengine wanahitaji kusafiri lakini hawana vyeti vya kusafiri. Wapo ambao hawana vyeti vya kuzaliwa. Hii sheria itawasaidia sana kupata stakabadhi hizo. Kule vijijini tunakotoka, wako wazee ambao kwa kweli hawana stakabadhi nilizozitaja. Hata wale ambao walipigania uhuru wa taifa hili, hawana stakabadhi hizo. Kuna bima ya kuwakinga wazee. Kaunti itakuwa na jukumu kubwa ya kuwasajili wale ambao hawako kwenye orodha ya Serikali Kuu. Kwa sasa, kuna wale wanaolipwa na Serikali kuu na wale ambao hawalipwi. Ile njia ilitumika kupata yale majina, ninaitilia shaka. Katika eneo-Bunge langu, sio wengi wanaofaidika. Lakini kwa ajili ya hii sheria, watafaidika. Hii ni kwa sababu watakuwa wamesajiliwa na kujulikana wako wapi. Vipo vikundi vya kuwasaidia wazee kujimudu kimaisha katika jamii zetu. Wazee watakuwa na uhuru wa kujiunga na hivyo vikundi na vitawasaidia kutafuta hela za kujikimu na kujiendeleza kimaisha. Sisi huwasikiliza na kuwauliza mawaidha wazee. Watakuwa na mahali pa kukutana na kuzungumza. Aidha, maoni yao yatasikilizwa na serikali za kaunti. Huu Mswada unanuia kuwasaidia wazee ambao hawana mbele wala nyuma. Ni wengi ambao hawana mtu wa kuwasaidia. Wazee watajua kwamba wako na haki ya kufanya chochote kwa sababu hili taifa ni lao pia. Naunga Mswada huu mkono. Naomba tuupitishe haraka ili wazee wapate haki zao."
}