GET /api/v0.1/hansard/entries/971159/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 971159,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/971159/?format=api",
"text_counter": 249,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kilifi CWR, ODM",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Gertrude Mwanyanje",
"speaker": {
"id": 13245,
"legal_name": "Gertrude Mbeyu Mwanyanje",
"slug": "gertrude-mbeyu-mwanyanje"
},
"content": " Ahsante sana, Naibu Spika wa Muda. Nimesimama kuunga mkono Mswada huu. Mswada huu unanigusa sana. Mimi natoka maeneo ya Kaunti ya Kilifi na imeangaziwa pahali pakubwa sana kwa mauaji ya wazee, waganga na washukiwa wa uchawi. Ndio maana nimesimama kuunga mkono Mswada huu uliotoka Seneti ili tuone vipi tunaweza kuwasaidia wazee wetu. Mhe. Naibu Spika wa Muda, wazee wetu wanauwawa. Kule Kilifi wanashukiwa kuwa wachawi. Yaweza kuwa ni kweli au si kweli. Mtu akiwa mzee na awe na nywele nyeupe, anaonekana kuwa mchawi, haswa kule Kilifi. Haya yote yanatokea kwa sababu vijana wetu hawajaelimishwa pakubwa kwamba hao wazee ni wenye busara na ndio wanaotupa mawaidha. Kwa sababu ya ukosefu wa ajira kwa vijana, mzee akiwa na nywele nyeupe, kwa sababu ako na shamba ambalo ni mali yake, husingiziwa kuwa mchawi. Anauawa na vijana wananyakua mali yake ili waweze kujikimu kimaisha. Kule kilifi tuko na akina mama wazee ambao wameachiwa mali na mabwana zao. Wao pia huwekwa kwenye vikundi vya wachawi na waganga. Wanauawa ili vijana ama jamii iweze kunufaika na mali hiyo. Naunga mkono vipengee vyote ambavyo vimependekezwa katika Mswada huu. Kulingana na Ibara ya 57 ya Katiba yetu, wazee wako na haki ya kulindwa na kutunzwa."
}