GET /api/v0.1/hansard/entries/971160/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 971160,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/971160/?format=api",
    "text_counter": 250,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kilifi CWR, ODM",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Gertrude Mwanyanje",
    "speaker": {
        "id": 13245,
        "legal_name": "Gertrude Mbeyu Mwanyanje",
        "slug": "gertrude-mbeyu-mwanyanje"
    },
    "content": "Kuna pesa za wazee ambazo zinastahili kuwafaidi wazee wenye umri wa miaka 65 na zaidi. Iwapo itaanza miaka 60, itakuwa bora zaidi waweze kujikimu wenyewe. Wazee hao kule kwetu wanaishi maisha ya ufukara mkubwa. Tuko na nyumba kule Ganze. Mimi natoka sehemu ya Ganze, ambako kuna nyumba ya wazee kule Mlima wa Ndege. Wazee wale wamewekwa tu pale; hawapati usaidizi wowote kutoka kwa Serikali. Hawana chakula ama malazi. Ni Wabunge tu wanaochangia chakula na kukaa kwao. Haswa Mbunge wa Ganze angelikuwa hapa, ningelimuunga mkono. Ameweza kuwatunza wale wazee, ambao wamefurushwa kutoka kwa familia zao."
}