GET /api/v0.1/hansard/entries/971163/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 971163,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/971163/?format=api",
"text_counter": 253,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kilifi CWR, ODM",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Gertrude Mwanyanje",
"speaker": {
"id": 13245,
"legal_name": "Gertrude Mbeyu Mwanyanje",
"slug": "gertrude-mbeyu-mwanyanje"
},
"content": "Tuko na mpaka makanisa. Mimi ni mkatoliki. Wakatoliki wana nyumba za wazee na wanawatunza wazee, lakini sioni kama Serikali inatambua kuweko kwa nyumba za wazee. Wazee hao wanaweza kuingizwa kwenye ule mpango wa kuwatengea wazee pesa za kuwalinda. Tumekuwa na Mswada hapa uliopendekeza kwamba wafungwa ama washukiwa wa mauwaji walioko magereza watengewe Kshs1 bilioni nzima ili waweze kula na kutunzwa. Wazee wetu hawa, ambao hutubariki sisi na ambao wametutunza, hawana kiwango chochote ambacho wametengewa na Serikali kuweza kuwalinda. Naunga mkono kwa dhati Mswada huu. Nawaomba Wabunge wote waweze kuunga mkono Mswada huu ili wazee waweze kutunzwa. Pia, ningependa nyumba za wazee zijengwe katika maeneo Bunge yote ili wazee wote nchini waweze kulindwa. Ningependa pia wazee katika kaunti zote nchini walipwe pesa za uzee kila mwezi ili nao waweze kuishi vyema kama Wakenya wengine."
}