GET /api/v0.1/hansard/entries/971246/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 971246,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/971246/?format=api",
"text_counter": 336,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu CWR, JP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
"speaker": {
"id": 786,
"legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
"slug": "ruweida-mohamed-obo"
},
"content": " Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii ya kuchangia Mswada wa utunzaji na ulinzi wa wazee katika jamii. Wazee ni baraka. Naunga mkono kwa dhati huu Mswada. Nimeusoma na una mambo mazuri sana. Ni lazima tuwe na desturi ya kuheshimu wazee. Nchi zingine zinatushinda. Sisi hapa, tunapoenda katika mahoteli makubwa ndio utaona tabia ya kuheshimu wazee na watoto mwanzo kwa chakula, lakini kule nyumbani wengine hawana hiyo desturi. Ninawashukuru watu wa Lamu. Tunaheshimu sana wazee. Tunawashinda watu wa Kilifi. Kiliffi kuna mambo mengi yanayotokea juu ya wazee. Ningependa Kamati ijue kwamba Lamu kuna sehemu nyingi hazikufikiwa na mradi huu. Kwa mfano, sehemu za Basuba, kwa sababu ya changamoto ya usalalama. Wazee wako lakini hawakufikiwa na mradi huu. Nataka pia wajue usafiri, kama vile sehemu za Kiunga, ni mbali mpaka Lamu. Mtu mmoja anatumia Ksh5,000 kwa usafiri; kuenda Ksh2,000 na kurudi Ksh2,000, na alale huko kisha aende achukue pesa za miezi miwili, mbazo ni Ksh4,000. Huwa ni kama pesa hizo zinaharibiwa njiani. Kuna ma- agent ambao wanafaa kuwekwa. Lamu wamewekwa ma- agent wawili. Kwa sababu ya mazingira ya Lamu, inafaa wawekwe ma- agent zaidi ya wanne wakizingatia vile Lamu iko. Shilingi elfu mbili ni kidogo sana kwa wale wazee. Kamati inafaa ishughulike ili waongezwe pesa hizo. Kuna wazee wengine ambao wamefikisha miaka sabini lakini sasa hivi hawawezi kushughulikiwa kwa sababu usajili umefungwa. Hawatapata nafasi hiyo mpaka usajili ufunguliwe tena. Ahsante. Napatia mwingine nafasi."
}