GET /api/v0.1/hansard/entries/971322/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 971322,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/971322/?format=api",
"text_counter": 67,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Haji",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 26,
"legal_name": "Yusuf Mohammed Haji",
"slug": "yusuf-haji"
},
"content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia maombi ya Taarifa kutoka kwa Seneta Loitiptip. Kwanza, ningependa kumpongeza Sen. Loitiptip kwa kuleta swali hili katika Bunge la Seneti. Lamu kwanza ni kaunti ambayo iko mbali. Vile vile, ni kati ya kaunti ambazo tunaweza kusema zimetengwa mbali sana na uongozi wa kitaifa. Walimu wanaofanya kazi kule, ambao wanajifunza, ni walimu ambao wanajitolea kuhakikisha kwamba Wakenya wanaweza kupata elimu. Iwapo TSC itashindwa kulipa yale marupurupu ambayo walimu hawa wanastahili kulipwa kwa wakati, ina maana kwamba tunaendelea kuigandamiza Kaunti ya Lamu kutokana na kupata huduma za kisawa sawa katika nchi ya Kenya. Kamati inapoangazia swala hili, iangazie pia zile taasisi nyingine za kielimu ambazo ziko katika Kaunti ya Lamu ambazo zinapunjwa marupurupu kama vile wanavyopunjwa walimu ambao wako katika kaunti hiyo. Asante, Bw. Spika."
}