GET /api/v0.1/hansard/entries/971330/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 971330,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/971330/?format=api",
"text_counter": 75,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante, Bw. Spika. Ningependa kuongezea taarifa ambayo imeombwa na Sen. Loitiptip. Mpango huu wa scholarship upo kwa shirika la Kenya Maritime Authority (KMA), Mombasa. Kwa hivyo, ningependa wakati Kamati itaenda Lamu kuchunguza, ipitie Mombasa waulize ni wangapi ambao wamepewa scholarship kutoka kaunti za Pwani. Madhumuni ya mradi wa LAPPSET ni kuinua hali ya maisha ya wakaazi wa kaunti hizi sita. Kwa hivyo, KMA itueleze ni wangapi kutoka Mombasa au kaunti jirani wamefaidika na mradi wa ufadhili wa masomo. Tumeona kwamba wengi wanaopata ufadhili wanatoka sehemu zingine na kupuuza matakwa ya wenyeji."
}