GET /api/v0.1/hansard/entries/971509/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 971509,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/971509/?format=api",
"text_counter": 254,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Asante, Bw. Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii. Naunga mkono hii Ripoti ambayo imewasilishwa katika Bunge la Seneti na Mwenyekiti wa Kamati ya Barabara na Usafiri. Ni aibu kwamba zaidi ya miaka 50 tangu Kenya ipate Uhuru, tumejipata katika hali ya suitofahamu haswa katika upande wa uchukuzi. Hali hii imeathiri wafanyabiashara, wasafiri na wanaoishi katika sehemu hizo. Kulingana na Ripoti hii, kuna kilomita zaidi ya 20 ambazo hazijakamilika. Magari yanapewa kibali cha kusafiri baada ya siku mbili au tatu. Tunashuhudia hali hii kule Mariakani katika Kaunti ya Kilifi. Bw. Spika wa Muda, je, umewahii kusafari ukitumia barabara ya Nairobi- Mombasa? Wakati unapofika Mariakani, utawekwa mahali ambapo ni kilomita 20 au 25 hivi kabla ya kufika Mji wa Mariakani. Hili ni jambo la aibu kubwa sana kwa Kenya, ukizingatia kuwa tuna zaidi ya miaka 50 baada ya Uhuru. Hayo yote yanaletwa kwa sababu ya uzembe kazini, ukorofi na ufisadi. Ripoti hii inaonyesha kuwa wale wanaosafiri kwenda maeneo ya Uganda kupeleka mazao yao ya shamba ni wafanyabiashara. Wao huenda Uganda na baadaye kurejea huku. Kuna vijana wengi wanaosomea nchi ya Uganda na husafiri kutumia barabara kwa sababu hawana nauli ya ndege. Ni aibu kumpigia mwanao simu kutaka kujua kama alifika shuleni au chuoni kisha anakuambia bado yuko Malaba. Ukiuliza siku ya pili, anakuambia bado yuko palepale. Roho yako huchafuka na unabaki kujiuliza kile anachofanya Malaba. Makosa siyo yake bali ni ya Serikali ambayo imeshindwa kutekeleza majukumu yake ya kuhakikisha barabara zetu ziko katika hali nzuri."
}