GET /api/v0.1/hansard/entries/971512/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 971512,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/971512/?format=api",
"text_counter": 257,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Ripoti hii ni muhimu na imekuja wakati unaofaa. Kamati husika inafaa kufuatilia ili kuona kwamba barabara zetu za mipakani zimetengenezwa ili kurahisisha usafiri. Ripoti hii imegusia kidogo tu eneo ambalo ninatoka. Mhe. Rais Uhuru Kenyatta alienda kule na watu walifurahi sana. Aliahidi kuwa barabara ya Bamba kwenda Mariakani, Ganze hadi Mji wa Kilifi itatengezwa. Barabara hiyo ni muhimu sana kwa watu wa maeneo ya Kaloleni na Ganze. Barabara yenyewe imetengenezwa tu kuanzia Mariakani na ikakomea Bamba. Kwa wale wanaosafiri kuelekea Ganze na Kilifi, hali yao ya usafiri ni ya utata zaidi. Unaweza kutumia masaa manne mahali pa kilomita 40. Barabara kama hizo ziko chini ya KeNHA, taasisi ambayo inahusika hususan na barabara za kitaifa. Ni muhimu barabara hiyo ishughulikiwe na Serikali ya kitaifa kwa sababu ni kama serikali ya kaunti imeshindwa kuona ya kwamba wanaoishi Bamba ambao wanafanya biashara zao Kilifi wana usafiri mwema."
}