GET /api/v0.1/hansard/entries/971513/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 971513,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/971513/?format=api",
    "text_counter": 258,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Katika eneo lilo hilo kuna watu wengi sana. Watu wanazaana. Nadhani wanataka kuongeza idadi ya wananchi na leba katika nchi yetu. Akina mama wajawazito wanaoishi maeneo ya katikati ya Bamba, Ganze na Kilifi wanaweza kuathirika pakubwa kiasi kwamba mama au mtoto anayezaliwa anaweza kufa, ama wote wawili, kwa sababu ya kukosa usafiri wa haraka kwenda hospitali ya Bamba ama Kilifi. Ni aibu kwa Serikali yetu ya kwamba baada ya miaka karibu 60 tangu tupate Uhuru, mama anaweza kukosa usafiri wa kwenda kujifungua na afie barabarani. Bw. Spika wa Muda, ukiangalia maeneo ya eneo Bunge la Kaloleni, kuanzia Kaloleni, Maandani mpaka Chagua kwenda chini kabisa hadi Vipingo, hakuna barabara. Ukiona watu wa Pwani wamekasirika na wanateta ni kwa sababu kama hizi. Hatutaki maeneo fulani yawe na barabara nzuri na mengine hayana. Si kwamba barabara zilitengenezwa halafu zikaharibika bali hazipo. Ni jambo la kusikitisha sana kwamba kliniki ambazo ziko katika maeneo ya huko na hata pande za Malaba--- Ripoti hii imetueleza wazi kabisa kuwa katika mpaka wa Kenya na Uganda--- Ikiwa Uganda wanaweza kutengeneza barabara zao--- Ukitoka Namanga kwenda Dar-es-Salaam, barabara zao ni nywee. Hazina shida na sote tunaona kwa macho yetu. Ukitoka hapa uingie Namanga, utaona kiyama. Tumeachiwa upande wetu tutengeneze lakini bado hatujatengeneza zaidi ya kilomita 20 ilhali bado tunalalamika hapa. Watu wanaokwenda Namanga na Lunga Lunga hawana barabara. Ni jambo la kusikitisha kama nilivyosema hapo awali ya kwamba ni karibu miaka 60 tangu tupate Uhuru. Ukienda Tanzania, kupitia Msambweni, ni bahati yako kufika kwenye mpaka wa Lunga Lunga. Kwa hivyo taasisi zinazohusika na mambo ya barabara, kama vile KeRRA na KURA zinafaa zijue kuwa kuna baadhi ya serikali za kaunti ambazo hazina uwezo. Si upande wa mpaka wa Uganda na Kenya pekee. Barabara ya kwenda Lunga Lunga hadi Tanga pia ina shida. Huko Namanga, Wamaasai wanafanya kazi kwa bidii lakini wanapata ugumu wakitaka kwenda hospitali ya Namanga. Wengine haswa akina mama wanaotaka kujifungua, hufia barabarani. Hiyo ni aibu kwa nchi ya Kenya."
}