GET /api/v0.1/hansard/entries/971516/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 971516,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/971516/?format=api",
"text_counter": 261,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Kwa kumalizia, upande wa Rabai, kuna barabara ya kutoka Mazeras mpaka Kaloleni ambayo ilijengwa kwa miaka mingi sana. Ilijengwa zamani, zaidi sana ya miaka 20 iliyopita. Sasa hivi imeharibika kwa sababu ina mashimo kila mahali. Haijapanuliwa wala kufanyiwa ukarabati. Ni kama tu kichochoro. Kuna lami upande mmoja na ukivuka vibaya unaanguka. Hiyo ni aibu. Ripoti hii imeletwa katika Bunge letu la Seneti. Kwa hivyo, Kamati ya Barabara na Uchukuzi lazima ihakikishe kwamba hatua imechukuliwa na Serikali. Wanafaa kuhakikisha kuwa mapendekezo yote yanafanywa. Sisi tutakuwa nyuma yao kuona ya kwamba tumepitisha Ripoti hii na hatimaye hatua kuchukuliwa na Serikali."
}