GET /api/v0.1/hansard/entries/972/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 972,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/972/?format=api",
    "text_counter": 477,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 96,
        "legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
        "slug": "johnson-muthama"
    },
    "content": "Watu ambao nyumba zao zilibomolewa hawajui kama walikuwa wamezijenga katika ardhi ya Serikali. Wao walinunua ploti zao kihalali. Mimi mwenyewe nimepinga mara nyingi njama za unyakuzi wa mashamba ya Serikali. Jambo hili nilijadiliana na Waziri wa Ardhi. Nilimweleza vile watu fulani walijaribu kunihonga ili nikubali wavamie shamba la Serikali la ekari 1,600. Walijaribu kunihonga na zaidi ya Kshs50 milioni na ahadi ya ekari 300 ikiwa ningewakubali wanyakue zaidi ya ekari 1,600; mali ya umma. Nilikataa njama zao na nikamwandikia Waziri wa Ardhi barua juu ya kisa hiki. Kamwe siungi mkono wizi wa mashamba ya Serikali. Lakini watu hawa wa Syokimau na kwingineko walitoa wapi vyeti vya kumiliki mashamba yao? Je, kwani kuna Serikali mbili katika nchi hii? Kwa nini Serikali inatoa vyeti kwa mkono wa kulia na kuvikataa kwa mkono wa kushoto? Ikiwa stakabadhi hizi za kumiliki mashamba ni bandia, kwa nini Waziri hajaamuru uchunguzi ufanywe ili kubainisha ukweli wa mambo na maofisa fulani katika Wizara yake kuchukuliwa hatua kwa kutoa vyeti hivi?"
}