GET /api/v0.1/hansard/entries/972118/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 972118,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/972118/?format=api",
    "text_counter": 534,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Bura, JP",
    "speaker_title": "Hon. Ali Wario",
    "speaker": {
        "id": 252,
        "legal_name": "Ali Wario",
        "slug": "ali-wario"
    },
    "content": "Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda, tunapozungumzia uhuru wa mahakama, vifungu vya sheria 48, 49, 50 na 51 vinazungumzia kwa upana uhuru wa mahakama. Uhuru huu utatoka wapi iwapo Jaji Mkuu na majaji wa Mahakama Kuu ni watu wanangoja waajiriwe na Rais, Rais ambaye licha ya kuwa kiongozi wa taifa, ni kiongozi wa utawala? Kwa hivyo, mimi naona kuna chembe kubwa hapa. Uhuru wa mahakama ni ndoto mpaka tuwe na sheria maalum ambayo inawapa rasilimali bila kuomba. Jaji Mkuu anasimama hadharani akiomba apewe rasilimali. Sasa uhuru utatoka wapi wakati Jaji Mkuu hawezi kutekeleza wajibu wake wa kisheria mpaka aombe utawala umpe hela aweze kutekeleza kazi yake?"
}