GET /api/v0.1/hansard/entries/972119/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 972119,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/972119/?format=api",
"text_counter": 535,
"type": "speech",
"speaker_name": "Bura, JP",
"speaker_title": "Hon. Ali Wario",
"speaker": {
"id": 252,
"legal_name": "Ali Wario",
"slug": "ali-wario"
},
"content": "Kuna dhana potovu kule nje kwamba Bunge la Taifa ndilo linasimamia ugavi wa rasilimali za taifa. Kuna vipengele kadhaa katika sheria yetu vinavyoruhusu utawala kutumia pesa bila kupitia Bunge. Ni tamthilia uwezo wa Bunge kusimamia ugavi wa rasilimali. Ugavi wa rasilimali ni siasa. Ni mchakato wa siasa. Ndiposa kama mahakama inafanya kazi yake vilivyo, mifereji hufungwa ili wahisi kiu, walie na waombe ifunguliwe kidogo kwa mtiririko. Kwa hivyo, uhuru wa mahakama ni ndoto ambayo ni ngumu Wakenya kuifikia kwa sasa."
}