GET /api/v0.1/hansard/entries/972122/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 972122,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/972122/?format=api",
"text_counter": 538,
"type": "speech",
"speaker_name": "Bura, JP",
"speaker_title": "Hon. Ali Wario",
"speaker": {
"id": 252,
"legal_name": "Ali Wario",
"slug": "ali-wario"
},
"content": "Katika Tana River, kuna Mahakama Kuu moja kule Garsen. Tana River ni kilomita 88,000 mraba. Ili mtu aliye Balambala aweze kufikia Mahakama Kuu iliyoko Garsen, lazima asafiri kilomita 400. Access to justice kama walivyosema wahenga ni nadra. Ni vipi yule mtu aliye kilomita 400 atapata haki kweli? Ni vizuri tuwe na kifungu ambacho kitatoa uhuru wa rasilimali kwa mahakama. Uhuru wa mahakama hauwezi kupatikana hadi hapo watapokuwa na uhuru wa kupata rasilimali bila kutegemea taasisi nyingine. Hivyo basi, zile pesa wanazopata zichunguzwe. Hata zile zitakazoenda kwa utawala pia zichunguzwe lakini kuwe na uhuru. Tusifike kiwango cha kumdhalilisha Jaji Mkuu hadi kiwango cha kuomba ama atamani kujiuzulu. Taifa hili linategemea mahakama. Juzi kulitolewa hukumu. Jaji mmoja wa Mahakama ya Rufaa alisema kushika Wakenya siku ya Ijumaa ni dhuluma. Lile jambo la kushika watu Ijumaa linajulikana kama “kamata kamata”, likimaanisha kwamba watu walale jela jumamosi na jumapili bila kufika mahakama. Jaji Mkuu alisema ni dhuluma. Lakini, nani atamsikiza? Je, watekelezaji wa sheria wataheshimu mahakama? Ni kwa nini hawajaheshimu uamuzi uliotolewa kumhusu Miguna Miguna?"
}