GET /api/v0.1/hansard/entries/972144/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 972144,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/972144/?format=api",
    "text_counter": 560,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kisauni, WDM-K",
    "speaker_title": "Hon. Mbogo Ali",
    "speaker": {
        "id": 13383,
        "legal_name": "Ali Menza Mbogo",
        "slug": "ali-menza-mbogo"
    },
    "content": " Asante sana, Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii kutoa usemi wangu kuhusu Ripoti zetu za Mahakama. Kusema ukweli, ni jambo la kusikitisha na kutamausha kumwona Rais wa Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Kenya akiongea mbele ya wananchi akilalamika anavyonyanyaswa, anavyoonewa na anavyodhulumiwa. Hii haitoi taswira nzuri kwa Jamhuri ya Kenya kwa sababu Rais wa Mahakama ni mtu mkubwa sana katika Jamhuri yetu. Nakumbuka vizuri sana hivi majuzi tulipokuwa na sherehe ya kitaifa ya Mashujaa Day katika Kaunti ya Mombasa. Rais wa Mahakama Kuu alilalamika sana akisema hakutambuliwa wakati alifika katika sherehe kubwa za Serikali kama ile. Ikiwa tunashindwa kumtambua Rais wa Mahakama, je kweli tutaheshimu uamuzi wa mahakama? Yeye ndiye Rais wa mahakama zile. Ni lazima tufikirie jambo hilo kama Bunge, tuone vile tunaweza kusaidia mahakama zetu na kuzipa nguvu zinapofanya uamuzi wao. Maamuzi mengi yametolewa na mahakama zetu lakini hayasikizwi wala kutekelezwa. Jambo hilo linaonyesha madharau makubwa sana katika Jamhuri ya Kenya. Yale yanayofanywa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}