GET /api/v0.1/hansard/entries/972145/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 972145,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/972145/?format=api",
    "text_counter": 561,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kisauni, WDM-K",
    "speaker_title": "Hon. Mbogo Ali",
    "speaker": {
        "id": 13383,
        "legal_name": "Ali Menza Mbogo",
        "slug": "ali-menza-mbogo"
    },
    "content": "na mahakama yanaonekana katika ulimwengu mzima. Uamuzi uliotolewa na mahakama unasikiza ulimwengu mzima. Ikiwa uamuzi ule hauwezi kutekelezwa, ni kuumanisha kuwa hata wale waekezaji walioko nje ya Jamhuri ya Kenya wanahofia kuja kuekeza katika Jamhuri ya Kenya kwa sababu wanajua kesho wakiwa na shida wapelekwe katika mahakama na uamuzi utolewe, uamuzi ule hautatekelezwa. Jambo hilo linaonyesha picha mbaya sana ya Jamhuri yetu ya Kenya. Kuna kiongozi hapa ameongea, Mjumbe wa kule Bura, akisema kuwa siku hizi, ikifika siku ya Ijumaa, watu wanakamatwa. Inaitwa kamata kamata. Kamata kamata ni kule kushikwa siku ya Ijumaa. Kuna jaji alitoa hukumu juzi akisema hiyo ni dhuluma. Lakini kusema kweli, nani atasikiza dhuluma kama ile? Ijumaa itafika kesho kutwa na utasikia mtu fulani amekamatwa na awekwe rumande kuanzia Ijumaa hadi Jumapili kwa sababu siku hizo hakuna mahakama inafanya kazi katika Jamhuri ya Kenya. Atafikishwa mahakamani siku ya Jumatatu. Mahakama za Kenya zinapigwa vita kila upande. Zinapigwa vita na Bunge la Kitaifa lenyewe kwa sababu sisi ndio tuna uamuzi wa mwisho katika kupitisha bajeti. Leo Mahakama isipocheza vile tunavyotaka, tunasema kuwa kama hawawezi kufanya yale yanatakikana basi bajeti yao itakatwa. Naongea kama Mjumbe wa Kisauni. Sisi watu wa Kisauni, Mombasa na Pwani kwa jumla tumeumizwa sana na kesi za mashamba. Leo ukienda katika mahakama zetu kule Bura, Garsen, Malindi, Kilifi, Mombasa, Kwale na Taita utapata kuna kesi zaidi ya elfu sita zimerundikana pale kuhusu masuala ya mashamba. Yote hayo yameletwa na ukosefu na uchache wa majaji na mahakimu. Kama tulivyosikia, mara ya mwisho mahakimu waliajiriwa ilikuwa ni katika mwaka wa 2011. Miaka tisa baadaye, hakuna hakimu yeyote ameajiriwa kupunguza ule mrundikano wa kesi katika korti zetu. Ndio maana tumesema leo korti zetu zimepata picha mbaya. Korti zinatambulika kuwa na sheria mbili. Kuna sheria ya matajiri na sheria ya masikini. Ukiwa masikini, kesi yako inaweza kuenda miaka mitano au sita mpaka ukashindwa njiani na ukaachana na kesi ile. Kwa sababu gani? Labda korti iko kilomita 300 kutoka pale ulipo na unatakikana ufike pale utoe ushahidi. Lakini kwa sababu huna uwezo, utakwenda mara ya kwanza na mara ya pili mwishowe unaachana na kesi kama ile. Uamuzi unatolewa. Mambo hayo yameleta picha ambayo inaonyesha mahakama zetu zinapendelea upande fulani. Lakini ukweli ni kuwa mahakama zetu hazipati fedha za kutosha za kuendeleza kazi zao. Juzi juzi tuliona mahakama nyingi zilisimamisha kazi zao kwa sababu hawakuweza kupata pesa za kulipia mafuta ya majaji kuenda kusikiza kesi kama zile. Hii ilionekana katika Jamhuri yote ya Kenya. Tuliona Malindi walifunga korti. Huku pande ya Kiambu korti ilifungwa kutokana na ukosefu wa hela ili mahakama zitimize wajibu wao wa kikatiba. Nilisikia ikitangazwa juzi kuwa mwaka jana, Mahakama ilikusanya ushuru wa Ksh700 milioni. Lakini leo unapata kuwa pesa wanazogawiwa kila mwaka zinazidi kupungua. Hatujui ni kwa nini zinazidi kupunguzwa. Tunajua kuna mikakati imewekwa kwa sababu uchumi haufanyi vizuri na tumepunguza hapa na pale lakini tunajua umuhimu wa mahakama zetu katika Jamhuri ya Kenya. Ni lazima kila Mkenya kuanzia Rais mpaka mtu wa kawaida aheshimu hukumu na uamuzi wa korti zetu za Kenya. Ukikumbuka mwaka wa 2017, Mahakama ya Upeo ilitoa uamuzi wakati wa kura ya urais kati ya Mheshimiwa Raila Amolo Odinga na Mheshimiwa Uhuru Kenyatta. Uamuzi ulitolewa kuwa ni lazima kura ile irejelewe kwa sababu kulikuwa na makosa fulani hapa na pale. Lakini viongozi wote - Mheshimiwa Raila Odinga na Mheshimiwa Rais Uhuru Kenyatta - waliheshimu uamuzi wa korti, kura ikarejelewa na mshindi akapatikana. Leo tuko na Mheshimiwa Rais Uhuru The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}