GET /api/v0.1/hansard/entries/972146/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 972146,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/972146/?format=api",
"text_counter": 562,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kisauni, WDM-K",
"speaker_title": "Hon. Mbogo Ali",
"speaker": {
"id": 13383,
"legal_name": "Ali Menza Mbogo",
"slug": "ali-menza-mbogo"
},
"content": "Kenyatta kama Rais wa Jamhuri ya Kenya. Ikiwa tulisikiza na kutii uamuzi ule mkubwa ambao ulikuwa ni wa Jamhuri nzima ya Kenya, kwa nini hatuwezi kusikiza haya maamuzi madogo madogo ambayo yanatolewa na kuhakikisha yametimia? Hiyo inaonyesha kuwa hatuko tayari kuitambua Mahakama kama kiungo muhimu. Huwa tunasema kuna viungo vitatu katika Jamhuri ya Kenya lakini kiungo cha Mahakama ni kiungo dhaifu. Kiko tu pale na watu fulani wanakichezea vile wanavyotaka. Lakini umefika wakati ni lazima tukubali kuwa mahakama lazima zisaidiwe na tuhakikishe zimejengwa kila sehemu ya Jamhuri ya Kenya. Leo Mombasa tunajenga mahakama nyingine. Ujenzi wa mahakama ile umesimama kwa sababu hakuna pesa ya kuendelea kujenga. Hii ni kumaanisha kutakuwa na mrundiko wa makesi kwa sababu mahakama hazitoshi. Tumesikia Mbunge wa Bura akisema mtu anatoka Mbalambala anasafiri kilomita 400 kuenda Garsen. Hiyo ndio korti iliyo katika eneo la ugatuzi la Tana River nzima. Eneo nzima liko na korti moja. Niambie kama mtu ataweza kufanya safari hiyo ya kilomita 400 afike mahakamani. Naunga mkono Ripoti hii. Lakini sisi kama Wajumbe tuna kazi kubwa ya kufanya ya kuhakikisha Mahakama yetu imepewa uhuru wa kufanya kazi zake kisawasawa bila kuingiliwa na upande wowote - sio Bunge wala upande ule mwingine. Naunga mkono Ripoti hii kikamilifu."
}