GET /api/v0.1/hansard/entries/973/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 973,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/973/?format=api",
    "text_counter": 478,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 96,
        "legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
        "slug": "johnson-muthama"
    },
    "content": "Ikiwa mtu anaweza kutengeneza stakabadhi bandia bila Wizara husika kujua, basi pengine cheti changu cha kumiliki shamba langu ni bandia. Pengine shamba langu tayari limeuzwa bila mimi kujua. Ni lazima mambo haya yachunguzwe kwa kina kirefu ili tujue ukweli wa mambo. Wananchi wengi wameteseka na kupoteza mali kwa sababu ya njama ya watu fulani, walagai wanaowahadaa kwa mashamba ya umma. Ni dhahiri shamba hili ni la shirika la ndege hapa nchini. Kwa hivyo, ninaiomba Serikali hii kuwafidia walioathirika na ubomoaji wa nyumba hizi kwa sababu makosa yalikuwa ya baadhi ya maofisa katika Wizara ya Ardhi. Tunajua watu hawa walinunua mashamba haya na wakajenga nyumba zao kwa gharama ya juu. Inafaa walipwe. Mwisho, ninamuomba Waziri atakapokuwa akitoa msimamo wa Serikali kuhusu jambo hili, atueleze vile watawafidia waathiriwa wa mkasa huu wa Syokimau na kwingineko. Ningependa kusikia jinsi watakavyo pata pesa za kuwafidia watu hawa. Ikiwa Serikali hii ina pesa za kupigana na maharamia wa Al Shabaab kule Somalia, kwa nini isipate pesa za kuwafidia watu wake?"
}