GET /api/v0.1/hansard/entries/973103/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 973103,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/973103/?format=api",
"text_counter": 60,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Zawadi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13176,
"legal_name": "Christine Zawadi Gona",
"slug": "christine-zawadi-gona"
},
"content": "Asante Bw. Spika, kwa kunipa nafasi hii ili kusema maneno machache kuhusu Malalamishi ambayo yako mbele yetu. Kwanza, nampongeza Sen. (Prof.) Kamar kwa kuleta Malalamishi haya kwa wakati ufaao. Ni kweli kabisa kwamba watu huwa na miungano kwa ajili ama kusudi la kunufaika. Nitapeana mfano wa Kilifi. Tulikuwa na mtambo wa korosho na kulikuwa na miungano ama co-operatives ambazo zilianzishwa wakati huo. Wengi ambao walikuwa wakichanga pesa walikuwa kina mama kwa sababu mtambo huo uliwaandika kina mama wengi sana. Hata hivyo, pesa yao ilienda hivyo na hakuna anayejua kwa kuwa mtambo wenyewe ulisambaratika. Wahenga walisema; yaliyopita si ndwele, tugange yajayo. Mambo yaliyoko mbele yetu yanafaa kutiliwa mkazo na kuchukuliwa ya muhimu. Kamati itakayohusika inafaa kufanya haraka kuhakikisha kwamba haitasambaratika kama vile zingine zilivyosambaratika. Vile vile, ningependa kuzungumza machache kuhusu EALA na pia kuwashukuru wafanyikazi wake kuja kututembelea. Nikiwa mwanakamati wa Kamati ya Uwuiano na Utengamano, nina jambo la kuzungumzia kuhusu Bunge letu la Afrika Mashariki. Hii ni kwa sababu tulitembelea Bunge lakini tuliwakosa waheshimiwa Wabunge kwa vile walikuwa likizoni wakati huo."
}