GET /api/v0.1/hansard/entries/973125/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 973125,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/973125/?format=api",
    "text_counter": 82,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Spika. Nashukuru ndugu zetu ambao wameweza kufika hapa kutoka Bunge la Afrika Mashariki wakiongozwa na Serjent-at- Arms, Bw. Migosi pamoja na Bw. Kikwae. Natumaini ndugu zetu wamejifunza mambo mengi katika Bunge la Seneti. Ni matumaini yangu kwamba wakirudi nyumbani, watapata ufahamu mzuri. Bunge la Afrika Mashariki ni Bunge muhimu sana kwetu sisi kwani huleta watu wote wa Afrika Mashariki katika kikapu kimoja ili tuwe na kuelewana na utangamano mzuri. Nawaomba wapeleke salamu zetu huko Jumuiya ya Afrika Mashariki. Tunaomba kwamba Bunge letu la Afrika Mashariki lizidi kudumu na kuleta uhusiano mwema katika Afrika Mashariki. Asante sana, Bw. Spika."
}