GET /api/v0.1/hansard/entries/973172/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 973172,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/973172/?format=api",
    "text_counter": 129,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika kwa kunipa fursa hii kuchangia Taarifa ambayo imeletwa Bungeni na Sen. Charargei. Ni jambo la kusikitisha kwamba NEMA imeamua kufunga Kiwanda cha Kusaga Miwa cha Kibos wakati ambapo wakulima wengi wanategemea kiwanda hicho kuuza miwa yao na kupata riziki ya kuwasomesha watoto wao ambao wako shuleni na vyuoni vikuu. Na pia kukimu mahitaji ya maisha. Ni lazima NEMA ifanye kazi katika hali tunayoita public interest au faida za jamii. Wajibu wao mkubwa ni kwa kusaidia umma kusonga mbele. Kwa hivyo, wanapofunga kiwanda wakati ambapo hakuna kiwanda kingine karibu na hapo ambapo wananchi wanaweza kupeleka miwa yao, ina maana kwamba wanajaribu kuhujumu haki ya umma kupata huduma sawa katika eneo lao. Kwa hivyo, kitendo hiki cha NEMA kinafaa kikemewe na hatua za haraka zichukuliwe. Hii kwa sababu wakulima wengi hawana matumaini hivi sasa. Viwanda vingi vya miwa katika eneo la Magharibi vimefungwa, kikiwemo kiwanda kikubwa cha Mumias. Kwa hivyo, wasiruhusiwe kuwadhalilisha wakulima ambao tegemeo lao kubwa ni kuuza miwa ili wapate mapato. Asante, Bw. Spika."
}