GET /api/v0.1/hansard/entries/973216/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 973216,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/973216/?format=api",
    "text_counter": 173,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Ni jambo la kusikitisha kwamba mwaka 2020 ulipofika tuliambiwa ya kwamba watu 3,000 wamepoteza kazi zao na wakulima zaidi ya 10,000 wamebaki na mimea ya miwa katika mashamba yao. Hawana mbele wala nyuma na hawajui waende wapi na miwa yao inaozea mashambani. Si vyema kutojali wengine wanavyoumia kwa sababu hatuna mashamba kule. Mtu aliye na ekari zaidi ya 10 za miwa sasa hajui afanye nini. Hakuna faida tena ya miwa kwa sababu itaozea kwa shamba."
}