GET /api/v0.1/hansard/entries/973222/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 973222,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/973222/?format=api",
    "text_counter": 179,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Najua kuwa wakulima ambao wamekuwa wakipeleka miwa katika Kiwanda cha Sukari cha Kibos wana majukumu mbalimbali. Sasa ufukara ama umasikini utaingia katika eneo hilo. Haya yote yanaletwa kwa sababu mashirika kama haya yanafanya mipango na mabepari. Kuna kampuni nyingine ambazo ziko huko na hakuna haja ya kuzitaja. Ni dhahiri kuwa ni mpango wa kufunga Kiwanda cha Sukari cha Kibos ili mwingine apate faida zaidi. Ikiwa huo ndio mpango, Seneti hii lazima isimame imara ili kuzuia mipango yote ya NEMA kufunga kampuni hiyo. Tunafaa kumwita Waziri anayehusika na ukulima aje hapa atueleze kama amekubaliana na mambo hayo. Watu wengine husema; kama si sasa, basi ni sasa hivi. Wahenga walinena: Chelewa chelewa, utapata mwana si wako. Kwa hivyo, ni vyema Seneti hii kuchukua hatua haraka ili kuhakikisha kuwa mpango huo umesimamishwa."
}