GET /api/v0.1/hansard/entries/973495/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 973495,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/973495/?format=api",
"text_counter": 43,
"type": "speech",
"speaker_name": "Matuga, ANC",
"speaker_title": "Hon. Kassim Tandaza",
"speaker": {
"id": 13287,
"legal_name": "Kassim Sawa Tandaza",
"slug": "kassim-sawa-tandaza"
},
"content": " Ahsante sana, Mhe. Spika, kwa kunipatia fursa hii kuwashukuru Wabunge wenzangu ambao niliweza kufika nao Msambweni jana. Wabunge wa nchi nzima, wa matabaka mbali mbali na dini mbali mbali waliweza kufika Msambweni kuweza kumsafirisha ndugu yetu, Mhe. Marehemu Suleiman Dori. Kama mnavyojua, sisi waislamu ukiaga, ukichukua masaa matatu kabla ya kuzikwa, basi huwa umechukua muda mrefu sana. Hili ni jambo ambalo ndugu zangu wa Bunge walifahamu. Kwa mfano, ikiwa nitaaga saa tisa, pengine ikifika saa kumi na moja nitakuwa nimezikwa. Kwa hivyo, nitawaambia wenzetu kwamba, kwa sababu tunajua kuwa tuna Wabunge waislamu, wawe tayari wakati wowote mwenzao akiaga kusafiri. Janga hili lilidhihirika kwa sababu kulikuwa na Waheshimiwa kutoka Magharibi mwa Kenya, Mlima Kenya na North Eastern . Mwisho, ningetaka kuwakumbusha wenzangu kuwa kwa desturi yetu, kwa matanga yetu hatuzungumzi mambo ya siasa. Huwa ni kuomboleza tu. Kwa hivyo, ijapokuwa najua tumezoea – hata sisi tumeweza kushiriki mazishi sehemu mbali mbali nchini, ambayo siasa ndio huwa mahali pake – kule kwetu, mambo kama hayo huwa hatuyazungumzii ijapokuwa mnajua kwamba sisi wapwani, ikiwa kutakuwa na shindano la kupiga domo kuzungumzia mambo ya siasa, hamtaweza kutushinda. Wakati wa mazishi huwa tunanyamaza tukiendelea kuomboleza kwa sababu hiyo ndio desturi yetu. Nawashukuru sana kwa misaada yenu, mchango wa kufika na pesa mlizoweza kutuletea. Kwa niaba yangu, familia na watu wa Kwale kwa jumla, tunawashukuru sana. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}