GET /api/v0.1/hansard/entries/973500/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 973500,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/973500/?format=api",
"text_counter": 48,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kinango, ODM",
"speaker_title": "Hon. Benjamin Tayari",
"speaker": {
"id": 13379,
"legal_name": "Benjamin Dalu Stephen Tayari",
"slug": "benjamin-dalu-stephen-tayari-2"
},
"content": " Asante sana, Mhe. Spika. Kusema kweli, kama wananchi wa Kwale na Pwani kwa jumla, tumesikitishwa sana na kifo cha mwendazake Mheshimiwa Suleiman Dori, ambaye alikuwa ni mpenda kazi, mpenda wenzake na mpenda nchi yake. Mheshimiwa Suleiman Dori, licha ya kuwa alikuwa Mbunge wa Msambweni, alikuwa rafiki wangu wa karibu. Tulizungumza mengi kuhusu maendeleo na kuhusu kazi yetu tunayoifanya na amesaidia sana Wabunge wengi wa kutoka Pwani kwa kuwaonyesha jinsi ambavyo watajifundisha maswala ya Bunge ili waweze kusaidia jamii kwa ujumla. Nataka niwashukuru sana viongozi wote walioweza kufika jana kwa mazishi, ijapokuwa muda ulikuwa mfupi. Familia imeshukuru sana kwa sababu, mwanzo, hawakutazamia kwamba watapata idadi kubwa ya Wabunge kuja kumsindikiza marehemu Suleiman Dori. Kwa niaba ya familia yangu na wananchi wote wa Kwale kwa jumla, nataka niiambie familia pole. Mwenyezi Mungu awape subira na heri wakati huu mgumu na Mwenyezi Mungi ailaze roho ya marehemu Suleiman Dori mahali pema panapo lala wema Asante sana."
}