GET /api/v0.1/hansard/entries/974185/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 974185,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/974185/?format=api",
    "text_counter": 72,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Boy",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13200,
        "legal_name": "Issa Juma Boy",
        "slug": "issa-juma-boy"
    },
    "content": "(ICU) hapo Aga Khan. Lakini nilidhani ni maradhi ya kawaida. Jana nikiwa nyumbani Vanga, nilipata taarifa kwamba Mhe. Dori alikuwa ameaga dunia. Nilijikokota kwa sababu hata saa hii ninaposimama hapa sijihisi vizuri, nikaandamana na viongozi wenzangu wa Pwani hadi Aga Khan tukatoa mwili na kuipeleka Gasi. Bw. Spika, Mhe. Dori alikuwa kijana shupavu ambaye alileta maendeleo katika Eneo Bunge la Msambweni. Ametengeneza barabara, mashule na kusaidia watoto wengi mayatima. Kwa hivyo, mimi kama Seneta wa Kwale nitamkumbuka Mhe. Dori kama Mbunge shupavu ambaye alichaguliwa mara mbili katika Eneo Bunge la Mswambweni ambalo sio kama maeneo mengine ya bunge. Alikuwa Mbunge mwenyemaono na aliyeleta maendeleo makubwa. Bw. Spika, umoja wetu ni nguvu. Kwa hivyo, tukipata nafasi, tuandamane twende Gasi kutoa salamu na rambirambi zetu kama viongozi. Kwa hayo machache, mniombee Mungu mimi pia, kwa sababu hali yangu sio nzuri."
}