GET /api/v0.1/hansard/entries/974197/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 974197,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/974197/?format=api",
"text_counter": 84,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa nafasi hii kuungana na ndugu zangu. Natuma risala za rambirambi kwa familia ya marehemu Mhe. Dori. Kwa niaba ya watu wa Kilifi, natoa risala za rambirambi kwa familia kwa sababu najua wana huzuni wakati huu. Itakumbukwa kwamba sisi Wabunge kutoka Pwani tulikuwa na kikao ili kumchagua kiongozi wetu. Kwa kauli moja, sote tulikubaliana kwamba marehemu Mhe. Suleiman Dori alikuwa na uwezo, akili na maarifa ya kuwa Mwenyekiti wa Wabunge wote kutoka Pwani. Hicho ni cheo ambacho tulimpa na sote tulikuwa tunamheshimu kama Mwenyekiti wetu. Sasa hivi, tuna jukumu la kujua nani atachukua nafasi hiyo. Alikuwa na ujasiri katika uongozi, utulivu, ukakamavu, na mwenye maono. Kwa hivyo, natoa rambirambi zetu kwa watu wa Msambweni. Sisi tutamkosa mwenzetu, lakini watakaomkosa zaidi ni watu wa Msambweni. Hii ni kutokana na juhudi zake hususan kwa upande wa kutengeneza shule, haswa shule inayojulikana kama Dori Girls’ Secondary School, ambayo niliiona kwa macho yangu. Ni shule nzuri sana na inasaidia watoto. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}