GET /api/v0.1/hansard/entries/975947/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 975947,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/975947/?format=api",
"text_counter": 329,
"type": "speech",
"speaker_name": "Wundanyi, WDM-K",
"speaker_title": "Hon. Danson Mwashako",
"speaker": {
"id": 13509,
"legal_name": "Danson Mwashako Mwakuwona",
"slug": "danson-mwashako-mwakuwona"
},
"content": " Asante, Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi nzuri ya kuchangia mjadala huu ambao umeletwa na mwenzangu wa Mwatate. Ningependa kumpongeza Mheshimiwa Mwadime kwa kutuletea Mswada mzuri kuhusu huduma za umma au public service kwa Kimombo. Itaangalia wananchi wote katika maeneo yote ya nchi na kuhakikisha kwamba kila mmoja anajihisi kuwa ana nafasi sawa ya uajiri katika nchi yetu. Katika Kenya hii Mungu alitubariki na makabila 43. Imekuwa jambo la kustaajabisha kuwa uajiri katika nchi yetu haujatilia maanani kila mmoja apate nafasi ya sawa. Naunga mkono Mswada huu. Kamati ya Uwiano na Utangamano huchapisha kila mwaka ripoti kuhusu jinsi idara za Serikali zimeajiri watu na kabila gani imeajiriwa zaidi kushinda nyingine. Ripoti ile huwa haitiliwi maanani na yeyote. Lakini leo, Mheshimiwa Mwadime ametupa nafasi nzuri kama Bunge kujadili maswala haya na kufanyia marekebisho sheria ili tuweke iwe lazima katika sheria kwamba ripoti hiyo itengenezwe na kila idara ya Serikali, kaunti na mashirika ambayo yanafadhiliwa na Serikali. Jambo hilo litatusaidia kujua ni watu gani wanaajiriwa zaidi na wagani hawaajiriwi. Itatusaidia kutoa ile kasumba ama ule uwoga kwamba kuna makabila ama sehemu fulani za nchi ambazo haziajiriwi. Wengi wanajihisi kwamba hatuna nafasi sawa. Kwa mfano, zamani kabla ya ugatuzi, kabla ya uchaguzi wa mwaka wa 2013, kuna maeneo ya nchi hii ambayo kila mara wangepata Waziri. Kila mara tungekuwa na wakurugenzi pamoja na makatibu kutoka sehemu zote za nchi. Lakini, leo hii, uajiri katika ngazi za juu umelenga maeneo fulani. Pia, unakuta kuwa kiongozi fulani anapewa nafasi ya uongozi kama mkurugenzi ama kama msimamizi wa rasilimali watu yaani human resource, ama katika ngazi za chini, utapata kuwa uajiri unalenga mahali anakotoka. Huwa kuna upendeleo na ukabila. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}