GET /api/v0.1/hansard/entries/975948/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 975948,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/975948/?format=api",
    "text_counter": 330,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Wundanyi, WDM-K",
    "speaker_title": "Hon. Danson Mwashako",
    "speaker": {
        "id": 13509,
        "legal_name": "Danson Mwashako Mwakuwona",
        "slug": "danson-mwashako-mwakuwona"
    },
    "content": "Nilikuwa ninazungumza na Mhe. Mwadime nikimweleza kuwa nitaleta mapendekezo ya marekebisho. Hoja hii haijataja vitengo vya usalama. Kwa kweli, jeshi na polisi huajiri vijana kutoka kila eneo bunge. Lakini, baada ya vijana hawa kuchukuliwa, wawe wawili ama watatu kutoka kwenye kata, bado huwa kuna watu ambao hujiunga na kikosi cha polisi ama jeshi kupitia milango ambayo imefunguliwa na wale wanaoshikilia nyadhifa za juu. Nitaleta mapendekezo ili jeshi na vitengo vinginevyo vya usalama navyo vituletee ripoti hizi."
}