GET /api/v0.1/hansard/entries/975949/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 975949,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/975949/?format=api",
    "text_counter": 331,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Wundanyi, WDM-K",
    "speaker_title": "Hon. Danson Mwashako",
    "speaker": {
        "id": 13509,
        "legal_name": "Danson Mwashako Mwakuwona",
        "slug": "danson-mwashako-mwakuwona"
    },
    "content": "Mhe. Naibu Spika wa Muda nitokako, najua Wabunge wengi wanakumbana na shida hii, vijana wanakosa tamaa. Wao huenda kwa wingi, mamia na maelfu, kupambana ili kujaribu kujiunga na vikosi vya jeshi ama polisi. Ni aibu kwa kuwa ni wawili ama watatu tu wanaochukuliwa kati ya vijana elfu mbili wanaojitokeza. Vijana hao huja kwetu sisi Wabunge kuomba wafanyiwe mipango. Zamani, Wabunge walikuwa wanapewa nafasi mbili au tatu kuwaingiza watu katika vitengo vya usalama—leo hii tunajua hali si hiyo. Maanake Wabunge tuko wengi, hatuwezi pewa nafasi hata moja kwa kuwa tutachukua watu bila hata kuenda kwa wananchi."
}