GET /api/v0.1/hansard/entries/975952/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 975952,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/975952/?format=api",
"text_counter": 334,
"type": "speech",
"speaker_name": "Wundanyi, WDM-K",
"speaker_title": "Hon. Danson Mwashako",
"speaker": {
"id": 13509,
"legal_name": "Danson Mwashako Mwakuwona",
"slug": "danson-mwashako-mwakuwona"
},
"content": "Katika kitengo cha Inland Container Depot hapo Mombasa vilevile, utakuta mambo yale yale. Kenya yetu, nashukuru kwa ajili ya handshake, BBI itaweza kutusaidia. Nikisikia mtu akisema hatuhitaji BBI, nashangaa maanake, suala hili tunazungumzia leo ni baadhi ya maswala ambayo yameangaziwa sana katika BBI. Kuna masuala ya kujihisi kuwa Wakenya; kupambana na ukabila; ukosefu wa kazi na shared prosperity . Wacha Mtaita wa Wundanyi aliyehitimu na shahada awe na nafasi sawa na yule Mkenya anayetoka Kisumu, Nyeri, Nakuru au Giriama ili Kenya iwe bora. Mtu anapoenda interview, wacha bidii yake na uzoefu wake wa kujieleza uwe ndio nguzo yake ya kumpatia kazi. Lakini isiwe kuwa, kwa sababu wengine hawana mkurugenzi wa kutoka sehemu yao, basi hawawezi kupata kazi. Nchi yetu inalia sana kwa sababu ya ukosefu wa kaziā¦"
}