GET /api/v0.1/hansard/entries/976128/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 976128,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/976128/?format=api",
"text_counter": 172,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Zawadi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13176,
"legal_name": "Christine Zawadi Gona",
"slug": "christine-zawadi-gona"
},
"content": "Najipongeza kama Seneta niliyekaa hapa, lakini bado sijatosheka. Kama vile Jakobo alikuwa anampenda Rachel, lakini hakumpata akampata Leah. Sio aliyekuwa amemtaka, lakini hakufa moyo; akarudi pale pale mpaka akampata Rachel. Nasi pia vile vile tuko hapa, lakini bado tuko na ari na mawazo ya kwamba kesho tutapata pale mahali tulipokuwa tukipataka. Sen. Wetangula, lako hilo nnakupa. Tuko hapa, lakini kisha baada ya muda, na sisi pia tutatoka tuwe na vile viti ambavyo twavitaka. Mwisho nikimalizia, Bw. Spika, nataka kumsifu mwanamke. Mwanamke amebobea mpaka kwa jua kali pia yupo; sio katika vyeo vikubwa tu, hata jua kali. Wanawake wamekuwa wabunifu, na wanafanya kazi zote ambazo mwanamke alionekana kuwa hawezi kufanya. Vile vile pia, vyama vyetu vya kisiasa pia vyafaa vituangalie. Mara nyingi mwanamke akisimama, anaulizwa iwapo ameolewa; ilhali mume haulizwi iwapo ameoa. Kwa hivyo, kuna sheria fulani ambazo bado zinatugandamiza kama wanawake katika jamii, na tunafaa tuziondoe. Mwanamke ni kiumbe, kama kiumbe yeyote mwingine, na anaweza kufanya kazi yoyote ambayo mwanamume anaweza kufanya. Kwa hivyo, tusibaguane kwa misingi wa kijinsia kwa sababu sote tuko sawa mbele za Mungu. Asante, Bw. Spika."
}