GET /api/v0.1/hansard/entries/976131/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 976131,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/976131/?format=api",
"text_counter": 175,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia hoja ya Seneta wa Nakuru, Sen. Kihika. Kwanza, nampongeza Sen. Kihika kwa kuleta Mswada huu kuadhimisha siku ya kina mama ambayo itakuwa tarehe nane, mwezi wa tatu mwaka huu. Ijapokuwa wanawake walipata matatizo mengi huko nyuma, sasa hivi tunaona kuna mwangaza umetokea katika vita vyao dhidi ya kubaguliwa; dhidi ya zile itikadi za zamani ambazo ni kinyume na maadili na kanuni; na vile vie pia dhidi ya ujinga. Wakati tulipopata Uhuru mara ya kwanza, tulikuwa tunapigana vita mbili; umaskini na ujinga. Kwa hivyo, tumeona kwamba wanawake wamepiga hatua kubwa katika vita dhidi ya mambo hayo. Bw. Spika, mbali na kuwa wanaume pia wanachangia kurejea nyuma kwa wanawake kwa sababu ya shida ambazo Sen. Zawadi amezungumzia, kwa mfano, kuulizwa iwapo ameolewa ama hajaolewa wakati anataka nafasi ya kisiasia, hiyo ni dalili kwamba unambagua mwanamke kwa sababu ya hali yake ya kijinsia. Kwa hivyo, lazima wanaume sasa wasonge mbele ili wahakikishe ya kwamba wasiwaache akina mama nyuma. Bw. Spika, nimefrurahi pia kwamba hivi majuzi, Serikali ya Uhuru Kenyatta ilimchagua msichana anayeitwa Nadia kutoka Mombasa - aliye katika wale ambao wako chini ya miaka 30 – kuwa ni Principal Secretary au Katibu wa Kudumu katika Wizara ya"
}