GET /api/v0.1/hansard/entries/976145/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 976145,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/976145/?format=api",
"text_counter": 189,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wario",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13224,
"legal_name": "Golich Juma Wario",
"slug": "golich-juma-wario"
},
"content": "Asante sana Bi. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii. Naunga mkono Rais wa Bureau of Women Parliamentarians of the Inter-Parliamentary Union(IPU), Sen. Kihika, kwa kuleta Taarifa hii kwenye Seneti. Nawaunga mkono akina mama hapa Seneti. Wanawake wanapaswa kuinuliwa katika nyanja zote za maendeleo. Wasichana na wavulana ni watoto katika familia. Tunapoinua wavulana, ni vyema tuwainue wasichana pia kwa sababu katika kujenga taifa dhabiti, lazima nguvu zote zitumike. Akina mama wakiwa na hafla yao, Maseneta wanaume wanafaa kuwaunga mkono. Wanawake hutulia zaidi wanaume wakiwa karibu nao. Wanaume wamekuwa wakiwaunga wanawake mkono katika mambo mengi. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}