GET /api/v0.1/hansard/entries/976702/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 976702,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/976702/?format=api",
"text_counter": 136,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wario",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13224,
"legal_name": "Golich Juma Wario",
"slug": "golich-juma-wario"
},
"content": "Asante, Bw. Spika kwa kunipatia nafasi hii. Nimesimama kuunga mkono Taarifa fupi iliyosomwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo ambako ninahudumu kama Mwanachama. Nzige wanaopatikana katika sehemu nyingi za nchi ya Kenya wameleta maafa mengi, hasa sehemu ninakotoka ya Tana River. Nzige wako kwa wingi. Tulipata baraka ya mvua nyingi hivi karibuni na sehemu zote zimekuwa na nyasi tele. Hasa mazingara yote yamekuwa ya kuvutia na maisha yetu pia imeanza kubadilika. Lakini tangu nzige watuvamie, mazingara hayo yameanza kuharibika. Nzige wamekuwa wengi na wanakula miche yote ambayo inakua wakati wa mvua. Nzige hawa wamesababisha ukosefu wa nyasi na kuathiri wakulima wanaofanya ukulima katika sehemu ya Mto Tana na wale wanaofanya kilimo cha unyunyizaji katika Mto Tana. Nilipoangalia katika Kaunti jirani, nzige wanapatikana kwa wingi. Kaunti hazina nguvu ya kupigana na nzige. Kwa hivyo, nzige wale wanaendelea kuzaa, kuwa wengi na kutapakaa katika sehemu nyingi. Kama Wizara husika haitachukua mikakati muafaka ya kupigana na nzige hawa, basi mvua ile ambayo ilikuwa baraka kwetu itabadilika na kuwa shida kubwa. Nawasihi Wakenya wote wakuje pamoja na kuomba Mungu. Hasa vile Seneta mwenzangu alivyosema, huu ni wakati ambao wanajeshi wa Kenya ambao wanaonekana kama hawana mambo mengi ya kufanya wanafaa kusaidia katika harakati za kupuliza madawa ya kuwaangamiza nzige. Hii itasaidia katika kupambana na uvamizi huu wa nzige. Asante kwa kunipa nafasi."
}